KANISA KATOLIKI LAVUNJA UKIAMYA WA SHA.
Published on 07/03/2025 08:03
News

Viongozi wa kanisa katoliki hapa Mombasa wamevunja ukimia wao kufatia atiati za mpango wa bima ya afya ya SHA humu nchini.Wakiongozwa na Askofu Martin Kivuva wakati wa kudhimisha jumatano ya majivu viongozi hao wametaja kuwa ni wajibu wa serikali kuangalia na kutatatua matatizo yanayowakabili wakenya kuhusu bima hiyo na wala si kukwepa majukumu yao.

"Kazi yetu si kupinga ila kuhimiza viongozi wetu kueka sawa maswala ambayo yanahitajika kwa wakenya ikiwemo mambo ya hospitali wakenya wengi wanaumia na kuhangaika kwahio kama kuna tatizo mahali acha lirekebishwe ili wakenya wapate huduma zinazofaa"

Hata hivyo askofu huyo amewaomba vijana kuwa makini zaidi hasa katika utafutaji wa ajira ili wasijipate mikononi mwa walaghai.

"Vijana wetu tunawaomba muwe wenye kuchunguza kwanza wakati mumeskia nafasi za ajira zimetangazwa mahali ili msijipate pabaya."

Comments
Comment sent successfully!