HATUTAKI SIASA ZA CHUKI.
Published on 07/03/2025 15:43
News

Wito umetolewa kwa viongozi humu nchini kukoma kutumia cheche Kali  za maneno zitakazo hatarisha Hali ya usalama nchini.

Akizungumza na wanahabari mwenyekiti wa dini ya kislamu hapa Mombasa Abu Qatada ametaja siasa za masimango na maneno  yasiyokuwa na maadili mema huchangia pakubwa kupotosha jamii na kuitaka tume ya kupambana na maadili NCIC kuingilia kati na kuwachukulia hatua wanaovunja sheria.

"Hatajafurahi kuona baadhi viongozi jinsi wanavyofanya katika swala la kukabiliana na tuanomba tume ya kupambana na maadili ya NCIC kuwachukulia hatua za kisheria viongozi wote wanaotumia maneno ya chuki."

Ni kauli iliyoungwa mkono na mkaazi wa Mombasa Hussein Ali, na kumtaka kamishna wa kaunti ya Mombasa kuhakikisha Hali ya usalama Iko imaara hususani Msimu huu wa mfungo wa ramadhani na kutaka shirika la usambazaji umeme Kenya power wajitahidi kuhakikisha wakaazi wanapata huduma za umeme Kila wakati bila hitilafu yoyote.

"Ni msimu wa mwezi mtukufu wa ramadhan kwa sasa na huu ndo wakati ambao sisi kama waislamu huwa tunaenda misikitini mara kwa mara hata usiku mkuu na itakuwa vyema kama swala la usalama na lile la umeme litazingatiwa"

 

Comments
Comment sent successfully!