Kombe la mabingwa barani ulaya zungumzia champions league itatamba tena usiku wa leo. Hapo jana tulishuhudia mihemko kaali kispoti pale ambapo intermillan waliwabandua Barcelona na kujipatia tiketi ya kucheza kwenye fainali.
Hivi leo, wanamizinga ama ukipenda wanabunduki Arsenal waalikwa ugenini kule Paris ufaransa na wenyeji PSG katika kinyanganyiro kikaali kusaka nani atacheza fainali.

Ikumbukwe kwamba mkondo wa kwanza Arsenal walipata adhabu bao moja komboa ufe, bao alilofunga kijana Ousmane Dembele mnamo dakika ya nne ya mchezo.Je Bukayo saka ataiweka arsenali kipao mbele ama ni Dembele ambaye atazidi kuwa mwiba kwenye ngome ya Asenali?. Tupatane kule parc Des princes nikupee uhondo wote wa spoti ndani ya Dayo radio viwanjani