Talanta zaidi ya talanta, miguso zaidi ya miguso, kinda wa wispanyola na winger wa Barcelona zungumzia lamine yamal amezua gumzo kwenye mashabiki wa kabumbu mbali mbali humu nchini na na mataifa mbali mbali. Kinda huyu mwenye umri wa miaka kumi na saba ameshinda Mataji mbali mbali ikiwemo taji la mchezaji mdogo wa mashindano mwaka juzi. Kule La Liga yamal amekuwa donda sugu kwenye timu pinzani kupitia mapande ya pasi, chenga na pia mashuti yake yalio na ubora na weledi wa juu.

Mabeki na walindalango wa timu tofauti tofauti hubabaika pindi tu wanapokumbana na kijana huyu. Nyota huyu atazidi kung'aa ama atazimwa na mastaa wengine?. Ungana na kikosi kizima cha Dayo radio viwanjani katika mazungumzo waziwazi kuangazia Talanta chipukizi katika ulimwengu wa spoti.