Askari Samuel Ndirangu Muchoki Maarufu kama Samido anatarajiwa kukamatwa baada wakati wowote endapo hatajiwasilisha katika kituo chochote cha polisi. Taarifa kutoka kwa Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) imetangaza kuwa Samidoh ni mtoro kazini.
Mwanamuziki huyo, ambaye ni afisa wa Polisi wa Utawala katika Kitengo Maalum cha Kukabiliana na Wizi wa Mifugo alishindwa kurejea kazini tarehe 27 Mei baada ya kumaliza likizo yake rasmi.
Kwa mujibu wa ripoti, afisa huyo amekuwa hayupo kazini kwa zaidi ya siku kumi bila ruhusa au sababu halali, jambo ambalo limepelekea kuchukuliwa hatua za kinidhamu.
Maafisa wa polisi katika kijiji chake cha nyumbani cha Gatumbiro, Kaunti ya Nyandarua, wameagizwa kumkamata mara moja endapo atakosa kujiwasilisha.
Awali Mwanamuziki huyo alihamishwa kutoka kituo cha polisi cha Nairobi hadi eneo la Bonde la ufa baada ya Nyimbo yake ya Wantam kuzua Gumzo kubwa mitandaoni