RATIBA YA LIGI KUU UINGEREZA
By Dayo Radio
Published on 19/06/2025 16:26
Sports

Safari ya kusaka atakaye jinyakulia taji la ligi kuu Uingereza ama ukipenda EPL itango'a nanga mnamo Tarehe 15/8/2025 huku timu mbali mbali zikimenyana na kukaragazana katika viwanja mbali mbali kwenye msimu wa 2025/2026. Mabingwa watetezi wa ligi hiyo msimu jana Liverpool watapaa ughani Anfield kuwakaribisha wageni Bournemouth kwenye mtanange wa kusisimua mwanzoni mwa ligi io. Haya yanajiri baada ya timu mbali mbali ku kuwasajili wachezaji mbalimbali kwenye Kambi zao huku zingine kukimbizana na wakati Ili dirisha la uhamisho wa wachezaji lisiwafungie nje. 

Ligi hii inatarajiwa kukamilika mnamo Tarehe 24/mei/2026. Je ni timu gani itakayoibuka mshindi na kujinyakulia taji hili? Ungana na kikosi kizima cha Dayo radio viwanjani utupee ubashiri wako kuhusu timu yako jinsi ilivyojiandaa msimu mpya unapobisha hodi. 

Makala ya spoti na Mbithi David

Comments
Comment sent successfully!