SERIKALI YAPUNGUZA BEI YA MBEGU ZA MAHINDI NA MBOLEA
By Dayo Radio
Published on 24/08/2026 13:09
News

Waziri wa Kilimo, Mutahi Kagwe, ametangaza kupunguzwa kwa bei ya mbegu za mahindi zilizoidhinishwa na mbolea kwa asilimia 50, hatua inayolenga kuwasaidia wakulima kukabiliana na hasara zinazotokana na ukame na kuendeleza uzalishaji wa chakula nchini.

Kulingana naye serikali itagharamia asilimia 50 ya gharama ya mbegu za mahindi zilizoidhinishwa, hivyo kupunguza bei kwa mkulima kutoka shilingi 300 hadi shilingi 150 kwa kilo.

Aidha, bei ya mfuko wa mbolea wa kilo 50 itapunguzwa kutoka shilingi 2,500 hadi shilingi 2,000 kwa wakulima watakaonufaika na mpango huo.

Serikali inatarajiwa kutumia takribani shilingi bilioni 6 katika ruzuku hiyo, huku mpango huo ukilenga kuwezesha upatikanaji wa takribani kilo milioni 40 za mbegu za mahindi.

Kagwe amesema wakulima wataweza kupata mbegu na mbolea hizo kwa bei ya ruzuku kupitia njia za usambazaji zilizoteuliwa na serikali.

Hatua hiyo inafuatia tangazo la Rais William Ruto kwamba serikali itapunguza bei ya mbegu za mahindi kwa asilimia 50 kuanzia Septemba 2026.

Comments
Comment sent successfully!