MASAHABIKI VS MARIOO BAADA TUZO ZA TRACE AWARDS
Published on 02/03/2025 11:25
Entertainment

Baada ya Tuzo za Trace, mashabiki wengi walimkosoa msanii Marioo wakidai kuwa hakufanya vizuri kwenye maonyesho yake. Marioo aliimba nyimbo Mbili "Nairobi" na "Unanichekesha".

Kujibu lawama hizo, Marioo ameposti video ya maonyesho yake ya moja kwa moja aliyofanya siku aliyopokea plaki na @audiomackafrica kwa kufikisha mitiririko milioni 100 kwenye mtandao.

 

Maonyesho hayo yalikuwa mazuri sana, tofauti na yale ya Tuzo za Trace, licha ya kuimba nyimbo zilezile.

Comments
Comment sent successfully!